Pata habari mbalimbali za Kitaifa,Kimataifa,Michezo na Burudani Kupitia blog yako ya ukweli na uhakika BORN IN DAR

Jiwe kali wiki hii! C pwaa-Mmhh! (HD)

Saturday, February 13, 2010

MISS TANZANIA 2009 KIZIMBANI! February 12, 2010
Zipo habari ambazo huwa mara nyingine sipendi hata kuziandika.Lakini kwa sababu kuandika na kukupa wewe msomaji taarifa mbalimbali hususani zinazowahusu “celebrities” wa kwetu na hata wa pande zingine za dunia,ndilo jukumu mama la BC,sina budi.Ni wajibu.
Mojawapo ya habari hizo ni hii ifuatayo.Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mrembo wa Tanzania kwa mwaka wa 2009(Miss Tanzania 2009),Miriam Gerald pamoja na rafiki yake wa kiume(boyfriend) anayeitwa Kennedy, leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na shtaka la kufanya vurugu na kuharibu mali za Bendi ya muziki ijulikanayo kama Volcano Sound ambayo inamilikiwa na Taji Mbaraka(mtoto wa gwiji la muziki Tanzania,Hayati Mbaraka Mwaruka Mwinshehe). Vurugu hiyo ilifanyika katika ukumbi wa TPDC uliopo Mikocheni.
Mashtaka dhidi ya mrembo huyo aliyetuwakilisha kule nchini Afrika Kusini miezi kadhaa iliyopita katika kipute cha urembo wa dunia(Miss World) ilifunguliwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay na kupewa jalada lenye namba za kumbukumbu OB/RB/2267/010 likiwa limepambwa na shtaka la Kuharibu Mali na Shambulio.

Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald(kulia) na boyfriend Kennedy wakiwa mahakamani hivi leo.Picha na Mroki Mroki
Ingawa kila mshtakiwa hana makosa mpaka hapo mahakama itakapothibitisha(innocent until proven guilty) ni wazi kwamba habari kama hizi sio nzuri kwa sio tu Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Uncle Hashim Lundenga,bali pia kwa umma wa watanzania na hususani vijana wadogo ambao wanawaangalia celebrities wetu kama role models. Tusubiri tuone itakuwaje.

No comments:

Post a Comment

toa maoni yako kadri uwezavyo.