Pata habari mbalimbali za Kitaifa,Kimataifa,Michezo na Burudani Kupitia blog yako ya ukweli na uhakika BORN IN DAR

Jiwe kali wiki hii! C pwaa-Mmhh! (HD)

Saturday, January 23, 2010

HUYU NDIYE MWAKILISHI WETU MNET FACE OF AFRICA January 22, 2010
Binti au mrembo unayemuona pichani anaitwa Lilian Mduda(21). Huyu ndiye mwakilishi wetu katika fainali za shindano la kumsaka Kisura wa Afrika kupitia Mnet(Mnet Face of Africa) zinatarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria tarehe 6 Februari/2010. Jumla ya warembo 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ndio waliofanikiwa kuingia katika fainali hizo na kwa maana hiyo ndio wataochuana.
Warembo wengine waliofanikiwa kufikia fainali wanatoka katika nchi za Angola,Ethiopia,Ghana,Kenya,Mozambique,Nigeria,South Africa,Zambia na Zimbabwe.
Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisomea Biashara(B.Comm), amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo.
Lilian anapenda kusoma novels zenye hadithi za kimapenzi na chakula akipendacho ni wali na maharage.Ndoto zake ni pamoja na kuweza kutembelea jiji la Paris siku moja.Pia anapenda mpira wa kikapu(basketball) na hupenda kusikiliza mziki na kujisomea.Kila la kheri Lilian.
Ukitaka kujua zaidi kuhusu Mnet Face of Africa na warembo wengine wanaoshiriki,bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment

toa maoni yako kadri uwezavyo.