Pata habari mbalimbali za Kitaifa,Kimataifa,Michezo na Burudani Kupitia blog yako ya ukweli na uhakika BORN IN DAR

Jiwe kali wiki hii! C pwaa-Mmhh! (HD)

Tuesday, March 2, 2010

ZA MWIZI 40,UKIMFUMANIA UTAFANYAJE?
Za mwizi arobaini. Bila shaka ushausikia msemo huo.Sina uhakika sana na idadi ya siku (40) lakini nina uhakika kwamba msemo huo humaanisha kwamba uovu una kikomo.Ipo siku utakamatwa.Inaweza kuwa sio ndani ya siku arobaini(40) lakini ipo siku tu!
Lakini inakuwaje siku ukimfumania mtu ambaye haibi kunde na choroko zako shambani bali anaiba penzi au mpenzi wako? Utapigana au utamuacha aende zake.Yaani namaanisha utayamaliza kistaarabu tu au mtaani patakuwa hapatoshi kwa vurumai au songombingo utakalolianzisha?
Sijui utafanyaje…lakini Hussein Machozi(pichani) anasimulia jinsi siku za mwizi(wa penzi,mali au hali) zinavyofikia ukingoni.Baada ya siku arobaini mambo yanawekwa hadharani.Tyler Perry,yule muongoza sinema maarufu kutoka nchini Marekani,anao mchezo(play) unaoitwa What is Done In The Dark…Must Come Out to Light. Labda Hussein Machozi anamaanisha hivyo pia.
Wimbo unaitwa Za Mwizi 40,unapatikana katika album yake ya Kwa Ajili Yako. Hii ni single yake ya 3 kutoka katika album hiyo, single mbili zilizotangulia ni pamoja na Kwa Ajili Yako na Utaipenda.Usikilize hapo chini;
SONG’S DETAILS
Track Name: ZA MWIZI 40
Singer: HUSSEIN MACHOZI
Produced by: AMBA & KID BWOY
Written by: HUSSEIN MACHOZI
Song Arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS

No comments:

Post a Comment

toa maoni yako kadri uwezavyo.