MIAKA 45 TANGU ALIPOFARIKI MALCOM X
zero
→ February 22, 2010 → Tags: In Memory/Kumbukumbu, Special Interest News →
Posti hii nilitakiwa kuipandisha jana lakini sikufanikiwa maana jana nilifunga kiroho na kifikra ili kumkumbuka Malcom X, mpigania haki za watu weusi kule Marikani. Malcom X alizaliwa na kupewa jina la Malcom Little kisha akaamua kubadili “Little” na kuweka “X” kwa kile alichodai kuwa jina la awali lilikuwa ni la kikoloni na lenye nia ya kuiba utu wake. “X” inasimama kama “Aliyepotea/Asiye na Jina” ikimaanisha Mwafrika aliyepoteza utambulisho wake baada ya kutekwa na kupelekwa utumwani kule Marikani.
Nimeona niweke posti hii ili tuelewe kwamba isingekuwa Malcom X na wengine waliotangulia kama Martin Luther King Jr., Mama Rosa Parks, au mapambano ya kuwakomboa watumwa ya Reli ya Ardhini” (Undeground Railroad) yaliyoongozwa na mwanamke mweusi Harieth Turbman, pengine Marekani ya leo isingekuwa na Rais Mweusi tunayemfahamu na kumshabikia, Barack Obama.
Malcom X alizaliwa katika familia yenye maisha duni na akiwa na umri wa miaka 13, baba yake ambaye alikuwa mpigania haki za watu weusi pia aliuawa na wazungu wabaguzi waliojulikana kama Ku Klux Klan (KKK), na mama yake alikuwa amefungiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili. Hivyo Malcom akaanza maisha ya kujitegemea akitumia wizi wa mifukoni kama njia ya kujipatia kipato.
Mwaka 1946 Malcom alifungwa jela kutokana na wizi. Akiwa Jela, Malcom ambaye hakuwahi kusoma vitabu akajikuta akiwa msomaji mkubwa wa vitabu ambavyo vilimwongezea maarifa aliyokuja kuyatumia baadae katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa watu weupe kwa watu weusi. (more…)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
toa maoni yako kadri uwezavyo.