Pata habari mbalimbali za Kitaifa,Kimataifa,Michezo na Burudani Kupitia blog yako ya ukweli na uhakika BORN IN DAR

Jiwe kali wiki hii! C pwaa-Mmhh! (HD)

Thursday, February 11, 2010

ALIYEKUWA DAKTARI WA MICHAEL JACKSON ASHTAKIWA KWA KIFO CHAKE.
Miezi saba baadaye,aliyekuwa daktari wa Mfalme wa Muziki wa Pop ulimwenguni,Michael Jackson, Dr.Conrad Murray ameshtakiwa rasmi kwa kifo cha mwanamuziki huyo maarufu ambaye katika maisha yake,aligusa wengi.Michael Jackson alifariki dunia tarehe 25 June mwaka jana akiwa na umri wa miaka 50.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Dr.Murray ambaye alifikishwa mahakamani mchana huu huko Los Angeles,amekana shtaka lake na ameachiwa kwa dhamana ya dola 75,000. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 5 April.
Ndugu wa Michael Jackson,kaka zake Jermaine,Tito,Jackie na Randy ,dada yake LaToya na wazazi wake Joe na Katherine walikuwepo mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
Hapo kabla Dr.Conrad Murray ambaye ni mzaliwa wa nchini Grenada,alikiri kwa polisi kwamba alimchoma Michael Jackson sindano ya dawa aina ya Anaesthetic Propofol kwa dhumuni la kumsaidia bingwa huyo wa Pop kulala.Alisema aliporudi tena chumbani alimkuta Michael akiwa hapumui.
Mchunguzi wa vifo wa Los Angeles alithibitisha baadaye kwamba dawa hizo ndizo zilizosababisha kifo cha Michael Jackson. Dr.Murray alikuwa ameajiriwa maalum kwa ajili ya kumuandaa Michael Jackson katika tour iliyokuwa ijulikane kama This Is It ambayo ilikuwa ianzie nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment

toa maoni yako kadri uwezavyo.