Pata habari mbalimbali za Kitaifa,Kimataifa,Michezo na Burudani Kupitia blog yako ya ukweli na uhakika BORN IN DAR

Jiwe kali wiki hii! C pwaa-Mmhh! (HD)

Thursday, March 4, 2010

OPEN LETTER FROM STIGGO IBRAHIM(S&S RECORDS)
Hey what’s up everybody! I thought the Producers in Tanzania have improved a lot but I guess I was wrong! Two and Half years ago, I made a beat and named it Block Running, I sold it to one of the Label called Koch Entertainment of New York with an agreement that wherever this beat goes my name gotta be there as a beat maker of this beat. Two days ago I was shocked when one of my friends from Tanzania sent me a song with the same beat I made 2 and half yrs ago! And I didn’t hear my name on the track. All I heard is Marco Chali.
So I called Koch Entertainment to ask what’s going on. Koch Entertainment management were so surprised to hear the news. So they told me to send the song to them and I did, they asked me if I ever sent the beat to MJ Records of Dar-es-salaam, Tanzania. I told them I never did but had put the beat on iTunes so people can buy and use it for promotions and not for any other type of business. But MJ Records used the beat without permission from Koch Entertainment and also they didn’t follow the agreement we signed that wherever this beat goes my name gotta be there as a beat maker!
I don’t have any rights of complaining this issue to MJ Records that why my name wasn’t on the song as a beat maker. All I will do is to take Koch Entertainment to court and they will deal with MJ Records. The only thing I am gonna deal with is if MJ Records bought this beat from iTunes. If they did why they used it for the business!!?
I put the song which Producer Marco Chali of MJ Records produced last year and my beat I made 2 and half years ago so you guys can compare and tell me if this beat is the same or not the same.Thanks.
Stiggo Ibrahim,
S&S Records-NY
Quick Rocka Ft QJ-Bullet
S&S Records & Koch Ent.
BC is trying to reach MJ Records for their comment.Stay Tuned.
UJUMBE KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS
Kwa wale ambao hawaupati mtandao wa www.globalpublisherstz.com; Wanashauriwa kubadilisha Browser na kutumia Mozilla Firefox.
Imeonekana kwa sasa website(tovuti) hiyo haifunguki kwa kutumia Browser ya Internet Explorer(IE).
Ni rahisi kubadilisha kutoka Internet Explorer kwenda Mozilla Firefox.Unachoweza kufanya ni ku-download Mozilla Firefox kwa kufungua link ifuatayo;
http://www.mozilla.com/en-US/products/download.html
Samahani kwa usumbufu wowote unaojitokeza kwa sasa.Tatizo linashughulikiwa.
GLOBAL PUBLISHERS
NAOMI CAMPBELL ANASAKWA NA POLISI
Mwanamitindo maarufu ulimwenguni,Naomi Campbell,yaelekea akaingia matatani tena kwani hivi sasa polisi wa jijini New York nchini Marekani,wanamsaka!
Naomi,ambaye mwaka jana alitua nchini Tanzania na kushiriki katika onyesho la hisani kwa ajili ya akina mama, safari hii anatafutwa akikabiliwa na shutuma za kumchapa vibao dereva wake huko New York.
Mwanamitindo huyo ambaye inasemekana ni mpenda ugomvi sio mgeni na vyombo vya usalama.Siku za nyuma amekwisha kutwa na hatia ya kumpiga mfanyakazi wake wa ndani jijini New York, kumpa kibano msaidizi wake jijini Toronto na pia kumwangushia kisago polisi ndani ya ndege katika uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London.Katika makosa yote hayo hapo juu,Naomi alikiri makosa yake na alihukumiwa kufanya kazi za kijamii(community services) kwa masaa zaidi ya 200.Kazi kweli kweli.Hivi kwanini kuna baadhi ya watu huwa wanadhani wanayo haki ya kuwaadhibisha watu wengine kiholela tu?Ni matunzo,jamii au?
NB:Hivi unajua Naomi Campbell alipokuwa mdogo alishiriki katika video ya Mfalme wa Reggae,Bob Marley katika wimbo One Love? Mtizame katika video hiyo hapo chini.Alikuwa na umri wa miaka 7 tu na hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa katika spotlight.

Tuesday, March 2, 2010

“I AM STILL GOOD AND WILL BE BACK SOON”-HASHEEM THABEET
When the news surfaced that, Hasheem Thabeet, is headed to the Development League (D-League), the reaction among Tanzanians especially the users of social networks such as Facebook and blogs were overwhelming. I guess the big question in lots of folk’s minds was; what is a D-League? Does it suggest that he is no longer going to be playing in the usual NBA league? Well, it depends on a lot of things. You can read more about the D-League and its implications or benefits to Hasheem career by clicking here and also here.
The social networks such as Facebook and blogs were immediately stuffed with comments and opinions. Some were wishing him a “quick comeback “to the NBA, while some couldn’t hesitate to throw jabs on him in the sentiment of “we told you”.
I guess the news was “worth the talk”, because not only Hasheem is the first Tanzanian ever to play in the NBA, but also the highest draft pick ever to go to the D-League. Thabeet, who has played sparingly in his rookie season, averaging 2.5 points in 10.3 minutes over 50 games, has been optioned to the Dakota Wizards. He made his debut yesterday when Dakota Wizards played Erie Bayhawks. Dakota Wizards won 108-103.
Before his debut in the D-League, I had caught up with Hasheem with only one question in my mind; about his reaction following the demotion to the D-League. This is how it went;
BC: Hasheem, what is your reaction to this whole thing of moving to the D-League?
HASHEEM THABEET: My reaction about D-League…Uhmmm… well I’m excited to participate in the D-League. I’m looking forward to playing and maximizing this opportunity to be on court and use the skills that I have developed thus far rather than to be on the bench.
Right now the key for me is consistency court time as I am still learning the Pro Game. I know Coach Hollins has my best interest at heart so I’m happy with his decision which I believe is to make sure that I stay active.
Now I know this is the time for the haters and all the doubters to talk and say whatever they have because they have been waiting to bring me down for a minute. So it’s my downtime and I promise I’m not backing back. It’s a new saga that has started. Plus I’m still be getting the same cheque… it’s not like they are not gonna pay me the usual. So I’m still good and soon I’ll be back!!! And oh by the way, I’m only going there for 6 games. So I will be back sooner than they are thinking.
**BC would like to wish Hasheem all the best in the D-League and eventually his return to the NBA.
ZA MWIZI 40,UKIMFUMANIA UTAFANYAJE?
Za mwizi arobaini. Bila shaka ushausikia msemo huo.Sina uhakika sana na idadi ya siku (40) lakini nina uhakika kwamba msemo huo humaanisha kwamba uovu una kikomo.Ipo siku utakamatwa.Inaweza kuwa sio ndani ya siku arobaini(40) lakini ipo siku tu!
Lakini inakuwaje siku ukimfumania mtu ambaye haibi kunde na choroko zako shambani bali anaiba penzi au mpenzi wako? Utapigana au utamuacha aende zake.Yaani namaanisha utayamaliza kistaarabu tu au mtaani patakuwa hapatoshi kwa vurumai au songombingo utakalolianzisha?
Sijui utafanyaje…lakini Hussein Machozi(pichani) anasimulia jinsi siku za mwizi(wa penzi,mali au hali) zinavyofikia ukingoni.Baada ya siku arobaini mambo yanawekwa hadharani.Tyler Perry,yule muongoza sinema maarufu kutoka nchini Marekani,anao mchezo(play) unaoitwa What is Done In The Dark…Must Come Out to Light. Labda Hussein Machozi anamaanisha hivyo pia.
Wimbo unaitwa Za Mwizi 40,unapatikana katika album yake ya Kwa Ajili Yako. Hii ni single yake ya 3 kutoka katika album hiyo, single mbili zilizotangulia ni pamoja na Kwa Ajili Yako na Utaipenda.Usikilize hapo chini;
SONG’S DETAILS
Track Name: ZA MWIZI 40
Singer: HUSSEIN MACHOZI
Produced by: AMBA & KID BWOY
Written by: HUSSEIN MACHOZI
Song Arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS

Tuesday, February 23, 2010

MIAKA 45 TANGU ALIPOFARIKI MALCOM X
zero
→ February 22, 2010 → Tags: In Memory/Kumbukumbu, Special Interest News
Posti hii nilitakiwa kuipandisha jana lakini sikufanikiwa maana jana nilifunga kiroho na kifikra ili kumkumbuka Malcom X, mpigania haki za watu weusi kule Marikani. Malcom X alizaliwa na kupewa jina la Malcom Little kisha akaamua kubadili “Little” na kuweka “X” kwa kile alichodai kuwa jina la awali lilikuwa ni la kikoloni na lenye nia ya kuiba utu wake. “X” inasimama kama “Aliyepotea/Asiye na Jina” ikimaanisha Mwafrika aliyepoteza utambulisho wake baada ya kutekwa na kupelekwa utumwani kule Marikani.
Nimeona niweke posti hii ili tuelewe kwamba isingekuwa Malcom X na wengine waliotangulia kama Martin Luther King Jr., Mama Rosa Parks, au mapambano ya kuwakomboa watumwa ya Reli ya Ardhini” (Undeground Railroad) yaliyoongozwa na mwanamke mweusi Harieth Turbman, pengine Marekani ya leo isingekuwa na Rais Mweusi tunayemfahamu na kumshabikia, Barack Obama.
Malcom X alizaliwa katika familia yenye maisha duni na akiwa na umri wa miaka 13, baba yake ambaye alikuwa mpigania haki za watu weusi pia aliuawa na wazungu wabaguzi waliojulikana kama Ku Klux Klan (KKK), na mama yake alikuwa amefungiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili. Hivyo Malcom akaanza maisha ya kujitegemea akitumia wizi wa mifukoni kama njia ya kujipatia kipato.
Mwaka 1946 Malcom alifungwa jela kutokana na wizi. Akiwa Jela, Malcom ambaye hakuwahi kusoma vitabu akajikuta akiwa msomaji mkubwa wa vitabu ambavyo vilimwongezea maarifa aliyokuja kuyatumia baadae katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa watu weupe kwa watu weusi. (more…)

Sunday, February 21, 2010

K’naan’s Waving Flags Is World Cup 2010 Official Song
Pamoja na ushabiki wote wa soka nchini ambao siku hizi umejikita sio tu katika timu za Yanga na Simba bali pia timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza(English Premier League), bado wengi tunakubaliana kwamba hakuna tukio la soka ulimwenguni linaloshinda mashindano ya kugombea Kombe la Dunia la Soka( Soccer World Cup).
Ubishi na ushindani wa Arsenal, Chelsea, Manchester United, Liverpool, Newcastle nk unapofikia ukingoni,macho na masikio huelekezwa katika Kombe la Dunia. Pale ndipo penye msisimko wa aina yake.Vipaji visivyo vya kawaida huonekana pale. Ndoto hutimizwa pale na pia ndoto huyeyuka au kuota mbawa na kupaa kama vile afanyavyo mwewe baada ya kukidakua kifaranga.
Kama unavyojua,mwaka huu kipute kipo barani kwetu. Hii ni mara ya kwanza kwa bara la Afrika kupewa nafasi ya kuandaa kombe la dunia. Ni mwaka ambao una matumaini mapya kwani ukitazama kwa makini,bara la Afrika lina wasakata kabumbu mahiri sana wanaocheza katika vilabu mbalimbali ulimwenguni hususani barani Ulaya.Mimi sina timu huko Ulaya;ila Real Madrid na Arsenal wakifungwa huwa sijisikii raha! Utaniita mshabiki?
Sasa kama ilivyo kwa matukio mengi makubwa ya michezo duniani,muziki huwa haukosi.Kunakuwa na wimbo maalumu kwa ajili ya mashindano(tournament’s official song). Kombe la dunia pia.Kwa mwaka huu, wimbo Waving Flags (kwa Kiswahili rahisi naweza kusema Kupeperusha Bendera) kutoka kwa mwanamuziki Knaan .Huu ndio World Cup 2010 Official Song.
Knaan ni mzaliwa wa Somalia. Kwa sasa makazi yake ni Toronto,Canada. Ni miongoni mwa wanamuziki wenye asili ya Afrika wanaofanya vizuri sana katika anga za muziki ulimwenguni. Bonyeza hapa ili kutembelea tovuti yake na pia hapa ili kusoma zaidi kuhusu historia yake.
Haya sasa,wimbo huo.Tupeperushe bendera.Je Afrika tutatoka kimasomaso huko Kusini mwa bara letu? Imebaki miezi michache.Usikilize wimbo Waving Flags hapo chini

Tuesday, February 16, 2010

Latest Films... COMMING SOON.... VERY SOON!

RJ- Tanzania Limited is a professional video production company that can help guide a client from concept and scriptwriting to shooting, editing and duplication. Whether you are looking for Professional Video, our production staff can help clients to produce effective programs and materials for marketing and other communications. We RJ-Tanzania Limited are very budget-minded and can work within the parameters given by our clients.
Not all production companies are alike. We pride ourselves on the high standards we put in all our work. The videos we produce will be ones you will be proud to have represent your company and your clients. In addition to providing turnkey productions, we also provide professional on-location production services anywhere in Tanzania, East and Central Africa.For out of town clients as well as production across the country and around the world. Send us an email for instant pricing.
Come todayRJ- Tanzania Limited.“Here we are to provide you a service of exceptional quality and value”

Monday, February 15, 2010

TUNAWEZA KUJIFUNZA NINI KUTOKA KWAO?
Kwa faida ya msomaji ambaye, kwa sababu moja au nyingine hawezi kuwatambua waliopo pichani; Kutoka kushoto ni Kenneth Kaunda,maarufu kama KK(Rais wa Zambia kuanzia mwaka 1964 mpaka 1991),Julius Kambarage Nyerere(Baba wa Taifa la Tanzania na Rais wake kuanzia mwaka 1964 mpaka 1985),Jomo Kenyatta(Rais wa Kenya kuanzia mwaka 1964 mpaka 1978.),Milton Obotte (Rais wa Uganda kuanzia mwaka 1966 mpaka 1971 na kisha mwaka 1980 mpaka 1985)
Je,wewe binafsi unajifunza au umejifunza nini katika kufuatilia jinsi walivyoendesha maisha yao,utumishi wao kwa umma nk? Unadhani kuna yepi ya msingi ambayo sisi kama wananchi na pia viongozi wetu wa hivi sasa tunaweza kujifunza kutoka kwa watu hao?Kumbuka mazuri na mabaya yao kwani kama tulivyo sote,they were not perfect,no one is!

Saturday, February 13, 2010

MISS TANZANIA 2009 KIZIMBANI! February 12, 2010
Zipo habari ambazo huwa mara nyingine sipendi hata kuziandika.Lakini kwa sababu kuandika na kukupa wewe msomaji taarifa mbalimbali hususani zinazowahusu “celebrities” wa kwetu na hata wa pande zingine za dunia,ndilo jukumu mama la BC,sina budi.Ni wajibu.
Mojawapo ya habari hizo ni hii ifuatayo.Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mrembo wa Tanzania kwa mwaka wa 2009(Miss Tanzania 2009),Miriam Gerald pamoja na rafiki yake wa kiume(boyfriend) anayeitwa Kennedy, leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na shtaka la kufanya vurugu na kuharibu mali za Bendi ya muziki ijulikanayo kama Volcano Sound ambayo inamilikiwa na Taji Mbaraka(mtoto wa gwiji la muziki Tanzania,Hayati Mbaraka Mwaruka Mwinshehe). Vurugu hiyo ilifanyika katika ukumbi wa TPDC uliopo Mikocheni.
Mashtaka dhidi ya mrembo huyo aliyetuwakilisha kule nchini Afrika Kusini miezi kadhaa iliyopita katika kipute cha urembo wa dunia(Miss World) ilifunguliwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay na kupewa jalada lenye namba za kumbukumbu OB/RB/2267/010 likiwa limepambwa na shtaka la Kuharibu Mali na Shambulio.

Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald(kulia) na boyfriend Kennedy wakiwa mahakamani hivi leo.Picha na Mroki Mroki
Ingawa kila mshtakiwa hana makosa mpaka hapo mahakama itakapothibitisha(innocent until proven guilty) ni wazi kwamba habari kama hizi sio nzuri kwa sio tu Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Uncle Hashim Lundenga,bali pia kwa umma wa watanzania na hususani vijana wadogo ambao wanawaangalia celebrities wetu kama role models. Tusubiri tuone itakuwaje.

Thursday, February 11, 2010

DANGER FID Q FEAT J BRYANT albumu mpya ya fid q iitwayo PROPAGANDA sasa ipo mitaani pata nakala yako sasa!
Siku chache zijazo,tarehe 25 mwezi huu kwa uhakika,Fareed Kubanda au maarufu kama Fid Q anatarajia kuiweka sokoni albamu yake mpya ambayo ameipa jina Propaganda.
Hivi karibuni ametoa single moja kama utambulisho wa kitachokuwepo katika album hiyo. Single inakwenda kwa jina la Danger akiwa amemshirikisha J-Bryant.Usikilize kwa kubonyeza player hapo chini.Usikilize kwa makini.Sikiliza midundo,hisia,ujumbe uliomo na kisha sema usikike.Kwa ufupi ninachoweza kusema ni kwamba kuna utofauti…
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser
CHID BEENZ KUMSHIRIKISHA T I D.

Yapo majina ya wasanii wa kizazi kipya ambao ukisikia wameshirikiana(collaborate)kutengeneza kazi fulani, basi unakuwa na imani kubwa kwamba kazi hiyo ina nafasi kubwa ya kuwa nzuri. Hiyo inatokana na uzoefu na pia zingatio za kazi zao zilizopita,nafasi waliyonayo katika uwanja mpana wa sanaa ya muziki na mambo kama hayo.
Hivi karibuni nilipoletewa kazi mpya na kuambiwa kwamba wasanii waliomo katika kazi hiyo ni TID(Top in Dar) na Chid Benz, nilikuwa na uhakika kwamba kazi hiyo itakuwa imesimama.TID na Chid ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao binafsi nawaheshimu na sioni noma kusema kwamba nazipenda nyingi kati ya kazi zao.Habari nzuri ni kwamba hawakuniangusha katika kazi hii ya hivi karibuni inayokwenda kwa jina Huyu.
Kama zilivyo kazi nyingi za wasanii wetu siku hizi,hii pia ni hadithi ya mapenzi (bado natamani wigo wa yaliyomo(content) za kazi za wasanii upanuke zaidi na kugusa maeneo mengine yanayoizunguka jamii).Kinachoufanya wimbo huu uwe tofauti ni uwezo binafsi wa wasanii husika na hadithi yenyewe.
Kazi hii imepikwa pale Tetemesha Records(kule kule alikoibukia Hussein Machozi) chini ya George Mpanda au maarufu kama Kid Bwoy. Bonyeza player hapo chini usikilize wimbo Huyu
BAADHI YA WASANII WANAMUZIKI WA MAREKANI WAKIFANYA REMIX YA WIMBO WA WE ARE THE WORLD WA HAYATI MICHAEL JACKSONI,baadhi ya wasanii ni kama usher raymond,celline dion...!
Miongoni mwa matukio ya ki-muziki ambayo yataendelea kukumbukwa kwa muda mrefu ni pamoja na tukio la jumla ya wanamuziki 45 kukusanyika katika studio za Jim Henson za jijini Los Angeles mwaka 1985 na kutengeneza wimbo ulioitwa We Are The World ambao ulikuwa mahsusi kwa kuchangia fedha kwa ajili ya Afrika na hususani nchi ya Ethiopia ambayo ilikuwa imekumbwa na ukame wa kutisha kuanzia mwaka 1984-1985.Ulikuwa ni umoja na upendo wa aina yake waliouonyesha wanamuziki wale sio tu kwa bara la Afrika bali kwa taasisi nzima ya ubinadamu. Wanamuziki Lionel Richie na Michael Jackson(RIP) ndio walioandika wimbo ule ambao ulifanikiwa kuchangisha jumla ya dola milioni 30 zilizokwenda kusaidia waathirika wa ukame ule.
Katika kujaribu kurudia kile walichofanya superstars wa ulimwengu wa muziki takribani miaka 25 iliyopita, hapo juzi jumla ya wasanii 100 (wengi wao kutoka Marekani) ambao wanatamba hivi sasa katika muziki ulimwenguni,walikusanyika katika studio moja chini ya Producer yule yule aliyefyatua We Are The World ya mwaka 1985,Quincy Jones ili kuutengeneza upya wimbo wa We Are The World(remake of We Are The World). Lakini safari hii sio kwa ajili ya kuchangia Afrika bali ndugu zetu wa Haiti ambao kama unavyojua wiki chache zilizopita nchi yao ilipata tetemeko la ardhi ambalo linahofiwa kwamba lilichukua maisha ya jumla ya watu 200,000.
ALIYEKUWA DAKTARI WA MICHAEL JACKSON ASHTAKIWA KWA KIFO CHAKE.
Miezi saba baadaye,aliyekuwa daktari wa Mfalme wa Muziki wa Pop ulimwenguni,Michael Jackson, Dr.Conrad Murray ameshtakiwa rasmi kwa kifo cha mwanamuziki huyo maarufu ambaye katika maisha yake,aligusa wengi.Michael Jackson alifariki dunia tarehe 25 June mwaka jana akiwa na umri wa miaka 50.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Dr.Murray ambaye alifikishwa mahakamani mchana huu huko Los Angeles,amekana shtaka lake na ameachiwa kwa dhamana ya dola 75,000. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 5 April.
Ndugu wa Michael Jackson,kaka zake Jermaine,Tito,Jackie na Randy ,dada yake LaToya na wazazi wake Joe na Katherine walikuwepo mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
Hapo kabla Dr.Conrad Murray ambaye ni mzaliwa wa nchini Grenada,alikiri kwa polisi kwamba alimchoma Michael Jackson sindano ya dawa aina ya Anaesthetic Propofol kwa dhumuni la kumsaidia bingwa huyo wa Pop kulala.Alisema aliporudi tena chumbani alimkuta Michael akiwa hapumui.
Mchunguzi wa vifo wa Los Angeles alithibitisha baadaye kwamba dawa hizo ndizo zilizosababisha kifo cha Michael Jackson. Dr.Murray alikuwa ameajiriwa maalum kwa ajili ya kumuandaa Michael Jackson katika tour iliyokuwa ijulikane kama This Is It ambayo ilikuwa ianzie nchini Uingereza.
AVATAR NA THE HURT LOCKER ZAONGOZA UTEUZI WA KUWANIA OSCAR
Unapoongelea sinema,hakuna ubishi kwamba majadiliano yako inabidi yaanzie Hollywood.Na unapokuwa Hollywood na kuamua kuanzisha mjadala wa Tuzo(awards) basi yakupasa uanzie kwenye tuzo maarufu za Academy au Oscars.
Muda mchache uliopita majina ya sinema,waigizaji,waongoza sinema na vipengele vingine walioteuliwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu yametangazwa. Kama ambavyo ilitarajiwa, sinema ya Avatar iliyoongozwa na James Cameron pamoja na sinema ya The Hurt Locker ambayo imeongozwa na Kathryn Bigelow(mke wa zamani wa James Cameron) ndio zimepata teuzi nyingi zaidi katika kuwania tuzo hizo maarufu ambazo zinafanyika kwa mara ya 82 (miaka 82). Movie hizo zimeteuliwa mara 9 au katika vipengele 9.
Shughuli za mwaka huu za tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 7 Mwezi Machi(takribani siku 33 zijazo).Zitaonyeshwa moja kwa moja(live) kupitia kituo cha televisheni cha ABC cha nchini Marekani.
Kwa orodha kamili ya Oscar Nominations kwa mwaka huu,bonyeza hapa. Je kuna movie,actor au actress ambaye ulitarajia angeteuliwa kuwania tuzo za mwaka huu ambaye hajatokea katika orodha?

Monday, January 25, 2010

MDAU MKUBWA WA BLOG YA BORN IN DAR kwa jina FINIASI yamo or RAYMOND YAMO!



MAUMIVU YA MIAKA”-WAGOSI WA KAYA January 24, 2010
Nina imani kwamba hujawasahau Wagosi wa Kaya.Naam ni wale wale vijana kutoka Tanga ambao miaka ileee waliingia kwenye anga za muziki kwa kishindo pale walipohoji “Tanga Kunani Pale”?
Tangu pale Wagosi wa Kaya wakawa wamejikita katika ile aina ya muziki wa kizazi kipya ambao mimi hupenda kuuita “conscious” kwa maana ya kwamba unalenga kwa undani kile kinachoendelea katika jamii.Ukipenda uite “muziki tambuzi”.
Baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa(hata wao wanakiri katika wimbo huu kwamba walikuwa kimya kwa muda mrefu) wamerudi.Na mara hii wamerudi wakiwa na timing ya aina yake.Wanagusia uchaguzi,siasa na mambo kama hayo. Kama unavyojua,mwaka huu,watanzania watajipanga foleni ili kuchagua tena viongozi.Demokrasia.Wao wanasema ni Maumivu ya Miaka 10!
Wasikilize Wagosi wa Kaya kwa kubonyeza player hapo chini.Sikiliza kwa makini ujumbe kwani kwa maoni yangu,kidogo sauti ya beats ni ya juu kuliko za wanaoghani.
JINSI YA KUSHINDA USAILI(INTERVIEW) YA KAZI→ January 24, 2010
Natumaini kwamba hujambo na unaendelea na mapambano ya maisha kwa ujasiri,bila woga wala dalili za kukata tama.Hivyo ndivyo inavyotakiwa.Kumbuka kwamba penye nia pana njia.Jifunze jambo jipya kila siku.Usipoteze muda bure.
Uchumi wa dunia bado haujatengemaa.Bado habari za makampuni kufungwa,kupunguza wafanyakazi,kufilisika na mambo kama hayo,tunazisikia na tutaendelea kuzisikia.Hatujui lini uchumi utarudia hali yake ya kawaida au tuseme ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.Hakuna anayejua kwa hakika.Hata Rais Obama hajui. Kilichobakia hivi sasa ni imani tu kwamba huenda kesho ikawa bora kuliko jana.Imani.
Kwa sababu ya kuyumba huko kwa uchumi,wengi wameshapoteza kazi zao na wengi zaidi wapo mbioni kupoteza.Lakini kupoteza kazi sio mwisho wa maisha.Kwa ufupi ukipoteza kazi uliyonayo hivi leo,huo ni mwanzo wa mbio za kutafuta kazi nyingine.
Kwa maana hiyo wengi wanaopoteza,kuachishwa au kuanza kutafuta kazi hivi leo,wanahitaji mbinu za kushinda mtihani wa usaili(interview). Leo nitaongelea jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya usaili,jinsi ya kujiongoza wakati wa usaili nk.
Kabla sijakuambia ninachotaka kukuambia,naomba nikwambie jambo moja la msingi.Ushindi katika jambo lolote hutokana na jinsi unavyojiamini.Kujiamini hata wakati wa usaili ni jambo la msingi na ambalo lazima ulizingatie.Lakini kumbuka kujiamini hakumaanishi kiburi,majivuno au maringo.Ninaposema kujiamini ninamaanisha kuwa na uhakika na unachokisema na kuonyesha kwamba una uhakika bila majigambo wala kiburi.
Umepata barua au simu kuhusu usaili.Zingatia yafuatayo;
Hakikisha umepata taarifa za kutosha: Mara nyingi upatapo barua au simu inayokuita kwenye usaili,mtu yeyote hujawa na furaha au msisimko wa ajabu.Ni ruksa kufurahi lakini kumbuka kuchukua taarifa muhimu(hususani kama habari hii inakujia kwa njia ya simu) kuhusu mahali utakapofanyiwa usaili(anuani,namba ya chumba,gorofa ya ngapi nk),muda na kama usaili huo utakuwa na watu zaidi ya mmoja au la.Taarifa kama hizo zitakusaidia katika kujiandaa.
Fanya uchunguzi kuhusu shirika/kampuni husika: Kabla ya kwenda kwenye usaili hakikisha kwamba umefanya uchunguzi wa kutosha kuhusu kampuni au shirika husika(research).Wanashughulika na nini,wateja wao ni kina nani,linamilikiwa na nani,lilianzishwa lini na kwa malengo gani.
Kama unamjua mtu au rafiki ambaye aliwahi kufanya kazi katika shirika au kampuni hiyo,mtumie ili kupata taarifa za ndani zaidi.Ufahamu wako kuhusu kampuni au shirika utawaonyesha wanaokufanyia usaili shauku uliyonayo kuhusu kampuni/shirika. Kumbuka tu kutojifanya unajua kupita kiasi.Bakia kwenye kiwango kinachostahili. (more…)

Saturday, January 23, 2010

C-PWAA…WHAT HAPPENED?

Pichani ni Ilunga Khalifa (CP) au kwa wengi C-Pwaa. Ana style ya kipekepekee hivi Bongo. Kuna wakati C-Pwaa alikuwa anablog kwa kutumia simu yake(mobile blogging).Yeye alikuwa msanii wa kwanza kuamua kuanzisha blog. Sina uhakika kwanini aliacha kwani kwa muda sasa blog yake imekuwa parking lot.What happened C-Pwaa?
PEOPLE’S CHOICE AWARDS:RED CARPET +CLEAN WATER
Nchini Marekani leo ni People’s Choice Awards. Sasa kwa wale wadau wa masuala ya fashion,urembo,vivazi nk, naambiwa kinachowavutia zaidi ni Red Carpet. Pale ndipo utaona nani kavaa nini,imetengenezwa na nani nk.Kumbuka tu kwamba wavaaji wale ambao ni celebrities,huwa wamepewa nguo,hereni,viatu vile nk kwa minajili ya kuzinadi.
Bonyeza hapa ili kuangalia mambo yalivyokwenda kwenye Red Carpet.
Nilichokipenda zaidi katika awards za mwaka huu ni kwamba kwa mara ya kwanza People’s Choice Awards zinachangia mradi wa Maji Safi kwa ajili ya watoto.Kwa kiingereza mradi huo unaitwa Children Safe Drinking Water. Celebrities wanapanda Mlima Kilimanjaro(nakumbusha Mlima upo Tanzania!) kwa ajili ya kuchangisha fedha. Tizama zaidi kuhusu mradi huu kutoka kwenye tovuti maalumu ya mradi huo.
Pichani juu ni Queen Latifah ambaye ndiye alikuwa Host kwa mwaka huu. As usual,I think she did a good job!
KARUME KUTOGOMBEA TENA;KATIBA HAIMRUHUSU
Rais wa Zanzibar Dr Karume ametangaza kutogombea tena uraisi katika uchaguzi ujao mwakani kwa kuwa katiba ya Zanzibar haimruhusu yeye kufanya hivyo.
Raisi ameyasema hayo hapo jana kwenye hotuba yake Kwenye sherehe za Miaka 46 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika kwenye viwanja vya Gombani Pemba ambazo zilihudhuriwa na na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwemo Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa,Rais Mstaafu Mzee Alhaj Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda,Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa,Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Sheif Sharrif Hamad pamoja na Lipumba,Waziri Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Nahodha na Wakuu wa Majeshi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Je unadhani nini itakuwa ni hatma ya Chama Cha Mapinduzi huko Zanzibar? Wakati wa CUF umewadia?Nani atamrithi Karume?
HUYU NDIYE MWAKILISHI WETU MNET FACE OF AFRICA January 22, 2010
Binti au mrembo unayemuona pichani anaitwa Lilian Mduda(21). Huyu ndiye mwakilishi wetu katika fainali za shindano la kumsaka Kisura wa Afrika kupitia Mnet(Mnet Face of Africa) zinatarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria tarehe 6 Februari/2010. Jumla ya warembo 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ndio waliofanikiwa kuingia katika fainali hizo na kwa maana hiyo ndio wataochuana.
Warembo wengine waliofanikiwa kufikia fainali wanatoka katika nchi za Angola,Ethiopia,Ghana,Kenya,Mozambique,Nigeria,South Africa,Zambia na Zimbabwe.
Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisomea Biashara(B.Comm), amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo.
Lilian anapenda kusoma novels zenye hadithi za kimapenzi na chakula akipendacho ni wali na maharage.Ndoto zake ni pamoja na kuweza kutembelea jiji la Paris siku moja.Pia anapenda mpira wa kikapu(basketball) na hupenda kusikiliza mziki na kujisomea.Kila la kheri Lilian.
Ukitaka kujua zaidi kuhusu Mnet Face of Africa na warembo wengine wanaoshiriki,bonyeza hapa

Thursday, January 21, 2010

SOUL LEGEND TEDDY PENDERGRASS IS NO MORE!!January 14, 2010
Kama wewe ni mpenzi wa muziki aina ya soul,bila shaka kabisa utakuwa unamtambua vyema mwanamuziki Teddy Pendergrass.
Habari za kusikitisha ni kwamba Teddy Pendergrass amefariki dunia hivi leo huko Philadelphia nchini Marekani.Kwa mujibu wa mtoto wake Teddy Pendergrass II, baba yake alifanyiwa colon cancer surgery miezi minane iliyopita na hakupona vizuri tangu hapo.Amefariki akiwa na umri wa miaka 59 katika hospitali ya Philadelphia’s Bryn Mawr.
Teddy ambaye nyimbo zake zilizojaa mahaba na bashashi zilitamba sana katika miaka ya 1970s na 1980s, alizaliwa March 26,1950 huko Philadelphia. Nyimbo kama vile “Turn Off The Lights”,”Close The Door” ni miongoni mwa nyimbo ambazo zilitokea kupendwa sana na mpaka hivi leo bado zinapendwa.
Teddy alitangaza rasmi kustaafu kutoka katika shughuli za muziki mwaka 2006 lakini akarudi tena jukwaani mwaka mmoja baadaye kwa ajili ya concert ya kuchangisha fedha kwa Taasisi yake ya Teddy Pendergrass Alliance inayosaidia watu walio na matatizo ya uti wa mgongo.
Kama utakumbuka Teddy Pendergrass mwenyewe alipata ajali mbaya ya gari mwaka 1982 ambapo aliumia vibaya uti wake wa mgongo kitu kilichosababisha alazwe hospitali kwa muda wa miezi sita.Baada ya hapo alirejea tena studio na kutoa albamu ya “Love Language”.
Pumzika kwa amani Teddy.Sikiliza wimbo wake “Close The Door” hapo chini.